Premier Bet
TMDA Ad

Top Stories

RC Makonda awajia juu Kinondoni “Rais ametoa pesa nyie mpo kwenye vikao” (+video)

on

Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda leo August 09 ametoa mwezi mmoja kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuhakikisha ujenzi wa maboresho ya fukwe za Coco unaanza mara moja na kama wakishindwa watanyang’anywa fedha hizo na kutafutwa mzabuni.

RC Makonda akiambatana na Katibu Tawala wa Mkoa huo wamefika kwenye ufukwe huo kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya mradi lakini wameshangazwa kuona hakuna chochote kinachoendelea wakati tayari Rais Dkt. John Magufuli alishatoa kiasi cha Shilingi Bilioni 14 za ujenzi huo lakini fedha hizo zimebaki kwenye akaunti bila matumizi huku watendaji wakilumbana kwenye vikao.

RC MAKONDA AMVAA MENEJA COCO “UNA WATOTO NA MKE MNATAKA UGOMVI”

Soma na hizi

Tupia Comments