Kumekuwa na malalamiko mengi ya kwamba Polisi wanawaonea raia, siku chache zilizopita kulikuwa na story ya tukio la Polisi kususiwa maiti ya kijana mmoja hapa TZ watu waliosusia maiti hiyo walidai Polisi walihusika kusababisha kifo cha mtu huyo, safarii hii imetokea Kenya.
Katika kaunti ya Nyeri nchini Kenya kuna tukio lililotokea jana March 26 ambapo watu waliokuwa wakiomboleza walichukua mwili wa mtu mmoja na kwenda nao katika kituo cha Polisi cha Mkurueni wakidai Polisi walihusika na kifo cha mtu huyo.
Waombolezaji hao walichukua mwili huo katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Nyeri na kuandamana hadi kituo hicho kwa madai mwanaume huyo alipigwa risasi na Polisi wa kituo hicho, walikutana na maafisa wa Polisi ambao walijaribu kuwazuia lakini waliwashinda nguvu na kuweka jeneza kwenye mlango wa kituo hicho na kuondoka.
Polisi waliwarushia mabomu ya machozi ili kuwatawanya, baadaye walikubaliana hali ikakaa sawa ambapo ndugu wa marehemu huyo walikubali kuuchukua mwili na kwenda kufanya mazishi.
Kusikiliza story hiyo iliyoripotiwa na kituo cha K24 bonyeza play hapa chini…
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>>twitter Insta Facebook