Duniani

PICHA 3: Kufanya mapenzi kwapelekea kobe kuwekewa matairi ya gari

on

Kila siku duniani vitu vya kushangaza na kustaajabisha vinaongezeka, leo nimekutana na hii ya huyu Kobe ambaye anaitwa ‘Bert’ na umri wake ukiwa ni miaka 22 ambaye anahifadiwa kwenye hifadhi ya Dinosaur Adventur, Norwich, kobe huyu ana kilo 100 na amewekewa matairi ambayo yanatumika kwenye gari.

Kobe huyu aliamishwa kutoka Afrika na kupelekwa Norwich, kuTokana na kuzalisha watoto wengi kutoka kwa kobe majike watano tofauti, walinzi waligundua kuwa kuna uvimbe kwenye miguu yake ya nyuma. Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na mtandao wa Independent imeelezwa kuwa kobe huyo alipata madhara hayo wakati akifanya mapenzi.

Wameongeza kuwa alipigana na kobe mwingine hivyo kupelekea kuchochea matatizo hayo na ili kumsaidia kutokana na madhara aliyoyapata kwenye migu yake ya nyuma walimwekea matairi.

VIDEO: Mambo ya kufahamu kuhusu kituo cha kisasa cha mabasi Morogoro, Bonyeza play hapa chini 

Soma na hizi

Tupia Comments