Michezo

Kocha afungiwa miezi sita na faini kisa kushangilia

on

Leo February 23, 2020 Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) limemfungia miezi sita na kumpiga faini ya Tsh. 500,000 Kocha wa timu ya Miembeni, Suleiman Mohamed kwa utovu wa nidhamu.

Kocha huyo alishangilia kwa kushusha suruali chini na kubaki na nguo ya ndani mbele ya mashabiki baada timu yake kushinda bao 1-0.

Adhabu hiyo iliyosainiwa na Katibu wa Kamati ya Mashindano ya ZFF, Hussein Ahmada, ni kwa mujibu kifungu namba 31 cha kanuni ya kuendesha mashindano hayo.

Hussein alisema Kocha huyo atatakiwa kulipa faini hiyo ndani ya kipindi anachotumikia adhabu hiyo na akishindwa kulipa faini adhabu itaendelea mara mbili.

LIVE: WAZIRI MKUU KASIM MAJALIWA ANAONGEA NA WACHIMBAJI WA MADINI NCHINI

Soma na hizi

Tupia Comments