Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Algeria Djamel Belmadi ameeleza malalamiko yake kwa mchezo wao wa mwisho wa kuwania kufuzu AFCON dhidi ya Tanzania kuchezwa Annaba Algeria.
Djamel ameeleza kuwa alisafiri kwa gari umbali wa saa 10 kutoka Algiers kwenda Annaba lakini ameona uwanja huo haufai kuchezea mechi na hajui kwa ni nini mechi imepelekwa huko.
“Niliendesha gari kwa saa 10 juzi kwa ajili ya kuja kuona miundombinu ya Annaba na kurudi, kiukweli hatuna chaguo sio Annab wala Costantine hakuna hata mzuri haupo kama ulivyokuwa June”
Septemba 7 2023 saa 22:00 EAT Algeria watacheza dhidi ya Tanzania, mchezo ambao Tanzania anahitaji ushindi au sare kufuzu AFCON huku Uganda anaombea Tanzania afungwe na Algeria na Uganda imfunge Niger ila hadi sasa katika Kundi F tayari Algeria ameshafuzu.