Michezo

Kocha Barcelona azidi kuandamwa

on

Mambo yanaendelea kumwendea vibaya kocha mkuu wa Barcelona Ronald Koeman baada ya timu hiyo kulazimishwa sare ya bila kufungana na timu ya Cadiz inayoshika nafasi za chini kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Hispania.

Katika mechi hiyo, kocha Koeman alipata adhabu ya kadi nyekundu baada ya msuguano na mwamuzi, huku kadi nyekundu nyingine iliyoleta mzozo na kuwapa wakati mgumu Barcelona ni Frenkie de Jong katika 75 jambo lililoipelekea Barca kucheza pungufu hadi dakika ya mwisho.

Barcelona kwa sasa inashika nafasi ya saba kwenye msimamo baada ya kucheza mechi tano ikiandika rekodi dhaifu ya kushinda mechi mbili pekee kati michezo yake.

Na katika mechi inayofuata, Barcelona inashuka dimbani ugenini kucheza dhidi ya Atletico Madrid Oktoba 2 mwaka huu.

LIVE: MAITI KUZUIWA KISA MILIONI 1.6, MUHIMBILI WAFUNGUKA “HATUDAI DENI LA MAITI, TUNADAI MATIBABU”

Soma na hizi

Tupia Comments