Michezo

Kocha kafukuzwa kazi kwa kupata ushindi wa 27-0

on

Moja kati ya habari inayosambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii ni pamoja na hii ya kocha wa kufutwa kazi na Rais wa Club yake  Invictasauro kutokana na kupata ushindi wa magoli 27-0.

Kocha Massimiliano Riccini wa timu ya Invictasauro U-18 ya nchini Italia iliyopo Grosseto katika mkia wa Tuscany, amefutwa kazi kufuatia timu yake ya Invictasauro U-18  kuifunga Marina Calcio 27-0.

Baada ya mchezo mkurugenzi wa michezo wa Marina Calcio  anayefahamika kwa jina la Tiberio Pratesi alilalamika kuwa timu ya Invictasauro, imeikosea heshima timu yake kwa kuifunga 27-0 na baada ya hapo alipokea simu kutoka kwa muwakilishi wa Invictasauro kuomba radhi kabla ya Rais wa club hiyo Paolo Brogelli kutangaza kumfuta kazi Riccini.

VIDEO: Ikitokea Taifa Stars ikacheza vs England, Bongozozo ataamua hivi dhidi ya taifa lake

Soma na hizi

Tupia Comments