Michezo

Kocha Micho awakata Chama na Chirwa Zambia

on

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Zambia Milutin Sredojevic “Micho” amewakata katika kikosi cha timu ya taifa ya Zambia wachezaji Clotous Chama wa Simba SC na Obrey Chirwa wa Azam FC kwa kudai wachezaji hao wameonesha utovu wa nidhamu kwa kushindwa kuungana na wenzao kama walivyotakiwa na kuachwa na ndege mara mbili.

“Tulitarajia wachezaji wawili kutokea Tanzania ambao walitakiwa kusafiri Jumatatu usiku, hata hivyo waliachwa na ndege na sasa wanaomba waje kesho, hiyo sio sawa wakati kuna mchezaji mmoja ambaye amewasifiri Kilometa elfu 10 kutokea Urusi yuko hapa na wao wako nchi jirani tu hapo sio sawa”>>> Micho

“Utovu huo wa nidhamu sitaruhusu kwa yoyote kuwa mkubwa kuliko nchi, nimeamua kuwaondoa katika mchezo huu hadi taarifa zaidi zitakopotolewa wakati mwingine”>>> Micho

Soma na hizi

Tupia Comments