Kocha wa Fenerbahce Jose Mourinho anakiri kupewa kibarua cha Uingereza mara mbili.
Meneja huyo wa zamani wa Chelsea anasema, hata hivyo, bado hajisikii kuwa tayari kuchukua kazi ya timu ya taifa.
“Nilikuwa na nafasi za timu ya taifa hapo awali, lakini kila mara nilizikataa. Nilipokea ofa kutoka Uingereza mara mbili lakini sikukubali,” Mourinho aliambia HT Spor.
“Si kazi itakayonifurahisha, mechi moja au mbili kwa mwezi, kusafiri kuangalia wachezaji, kusubiri mashindano… nina nguvu nyingi kwa sasa.
“Labda siku moja nikiwa mzee na nimechoka, lakini sio leo.”