Michezo

Kocha wa Gambia alalamikia upendeleo AFCON 2021

on

Kocha wa Timu ya Taifa ya Gambia Tom Saintfiet leo amefunguka na kuwatuhumu CAF kuwa wanapendelea mataifa ya makubwa katika michuano ya AFCON 2021 kwa kuwaweka hotel zenye hadhi ya nyota 5.

Tom amesema hayo nakudai kuwa mataifa ya anglophone (Zimbabwe, Malawi na Gambia) wamewekwa kwenye hotel za kawaida kiasi cha kufikia wachezaji wake 6 kushea chumba kimoja na baadhi ya staff wake kushea vyumba pia.


Hata hivyo CAF wamekanusha taarifa hizo na kudai kuwa CAF itagharamiwa jumla ya watu 40 tu na baadhi yao watashea vyumba watu wawili wawili, hivyo taarifa za wachezaji sita kushea chumba na choo wanazikanusha, japokuwa Kocha Tom amesimamia msimamo wake.

Soma na hizi

Tupia Comments