Wakati kukiwa na tetesi kuwa James Kotei wa raia wa Ghana anayeichezea Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini anahusishwa kujiunga na Yanga SC ya Tanzania.
Kocha wa Kaizer Chiefs Ernst Middendorp amesema kuwa hawezi kujibu kuhusiana na tetesi hizo kwani hajui hata mchezaji huyo alipo kwa sababu hakuwepo kwenye mazoezi ya Jumamosi na Jumapili.
“Kiukweli siwezi kukupa hata jibu sahihi ambalo litaweza kukuridhisha, (Kotei) hakuwa hata mazoezini asubuhi hii (Jumapili) na jana pia hakuwepo, hivyo jibu la kwanza sijui alipo”>>> Middendorp
Kotei ambaye amekuwa hapati nafasi ya kucheza toka ajiunge na timu hiyo, kwa mujibu wa mtandao wa goal.com unaeleza kuwa Kaizer Chiefs tayari wamepata mbadala wa Kotei ambaye ni mkenya Anthony Akumu aliyekuwa mchezaji huru kutoka Zesco ya Zambia, huku Zesco nao wakidai kuwa wanamuona Kotei kama mbadala wa Akumu.