Michezo

Kocha wa Simba SC kaweka wazi kuhusu stori za kuondoka

on

Kocha mkuu wa Simba SC Patrick Aussems amelazimika kuweka wazi taarifa zake binafs baada ya kuzuka kwa tetesi kuwa kuna uwezekano bodi ya wakurugenzi imemfungashia virago kocha huyo.

Aussems ameweka wazi kutokana na kukosekana kwake kwa siku mbili katika mazoezi ya Simba SC, hiyo inatokana na kuwa na mambo binfasi ndio yamemfanya aondoke na atarejea kesho kuiandaa timu yake.

Kupitia instagram Patrick Aussems ameandika hivi “Nililazimika kuondoka kwa siku mbili kwa sababu binafsi, nitarudi kesho kujiaandaa na mechi yetu dhidi ya Ruvu ili kupata point 3 zaidi”

VIDEO: BONDIA ARNEL TINAMPAY NAMBA 2 KWA UBORA PHILIPINE BAADA YA MANNY PACQUIAO KATUA DSM

Soma na hizi

Tupia Comments