Michezo

Kocha wa Simba SC Sven akalia kuti kavu

on

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Ghana Nuhu Adam ameripoti kuwa uongozi wa Simba SC haufurahishwi na mwenendo wa timu yao chini ya Kocha mbelgiji Sven Vanderbroeck Broeck na watakutana kuamua hatma yake katika mechi zijazo endapo matokeo yataendelea kuwa hivi.

Baada ya mchezo huo kocha wa Simba SC mbele ya waandishi wa habari alitoa kauli iliyotafsiriwa kama ni fumbo na inawezekana kukawa kuna kitu kinaendelea.

“Sifikiri kama tumefungwa sababu ya game fitness mhhh ni ngumu kwa wakati huu kutaja ni nini tatizo hususani kama utaeleza kila kitu katika vyombo vya habari”>>> Sven Vanderbroeck

Simba SC leo imefungwa mchezo wake wa pili mfululuzi baada ya ule wa kwanza kufungwa na Tanzania Prisons katika uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga kwa goli 1-0 na leo Ruvu Shooting wamewafunga tena 1-0.

Soma na hizi

Tupia Comments