Michezo

Kocha wa Uganda kataja tishio lao CHAN 2020

on

Siku chache zimepita toka shirikisho la soka Afrika CAF lipange makundi ya fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN), kocha wa timu ya taifa ya Uganda ya wachezaji wa  ndani Johnathan Mckinstry  ameeleza kuwa kwa sasa hofu yao ipo kwao wenyewe.

Johnathan Mckinstry ameeleza kuwa kwa sasa ataandaa timu itakayojitoa kwa asilimia 100 kuelekea michuano ya CHAN itakayofanyika Cameroon kuanzia April 4-25 2020,  katika droo iliyochezeshwa Jumatatu hii Uganda wamepangwa na timu za taifa za Togo, Morocco na Rwanda.

“Nafikiri tishio kubwa kwetu ni sisi wenyewe, tunataka kuhakikisha kwamba tunafanya vizuri kwa sababu tuna zaidi ya vipaji hapa Uganda, jitihada ya timu na maadili ya kazi ambavyo tumevionesha ni wazi kuwa tunaweza kuendelea na kujitoa kwa 10/10 sio tu katika mechi hata mazoezi kila siku”>>>Johnathan Mckinstry 

Soma na hizi

Tupia Comments