Michezo

Kocha wa zamani wa Sporting CP aipa onyo Man United kuhusu Bruno Fernandes

on

Kocha wa zamani wa club ya Sporting CP Carlos Carvalhal ameipa onyo Man United kuhusu matumizi ya mchezaji Bruno Fernandes aliyejiunga na timu hiyo January hii kuwa sio namba 10 bali ni kiungo japokuwa amekuwa akifunga (box-to-box midfielder).

“Anapiga, anafunga na anapiga vizuri mipira iliyokufa (free kick) ila sio namba 10 ni namba 8 (kiungo) box-to-box player  ambapo anaelewa sana mchezo sio tu anacheza anelewa kila kitu kinachomzunguuka”>>>Carlos Carvalhal

Bruno alijiunga na Man United dirisha dogo la January 2020 kama mbadala wa kiungo wa Man United Paul Pogba ambaye amekuwa na mejeruhi, Fernandes ameonesha kiwango kizuri katika mchezo wake wa kwanza wa Man United dhidi ya Wolves.

VIDEO: MASAU BWIRE ATOLEWA NA WANAJESHI, MASHABIKI WA YANGA WAMZONGA

Soma na hizi

Tupia Comments