Kocha mkuu wa Wekundu wa Msimbazi Simba Zdracko Logarusic amefikia makubaliano ya kuongeza mkataba na klabu hiyo utakaoendelea kumuweka Msimbazi kwa miaka mingine miwili.
Katika makubaliano hayo Logarusic atalipiwa nyumba maeneo ya Masaki,gari ya kutembelea,mafuta na posho ya kila siku huku pia mshahara wake ukipandishwa kufikia Zaidi ya dola elfu 5.
Pia Logarusic amepewa jukumu la kuleta kocha wa viungo ili kuwajenga wachezaji wa kikosi hicho katika harakati za kukiimarisha kikosi cha Wekundu hao.
Logarusic amekubali kuitumikia Simba huku klabu kutoka nchi mbalimbali zikimmezea mate ili kumnasa kwenye vikosi vyao.
Tayari GOR MAHIA wamegonga hodi kuhitaji huduma ya kocha huyo aliyewahi kuifundisha timu hiyo ya nchini Kenya ambayo kwasasa haina matokeo mazuri sana.
Mbali ya Gor Mahia klabu mbili za nchini GHANA na klabu moja ya MISRI nazo zinaendelea kufuatilia nyendo zake ikiwa pamoja na kumshawishi aachane na Simba na wako tayari kutoa dau nono.
Wakati huo huo kocha msaidizi wa klabu hiyo Suleiman Matola naye atafaidika kutokana na kuongezewa maslahi katika mkataba wake atakaopewa baada ya kuonekana ana ushirikiano mzuri na Logarusic baada ya kocha huyo kumpigia upatu wa kutaka kuendelea kubaki naye kama msaidizi wake.
SOURCE: SuperMario Blog