Michezo

Yanga SC imeondolewa na Zesco na kuangukia Kombe la Shirikisho

on

Wawakilishi pekee wa Tanania katika michuano ya CAF Champions League waliosalia katika msimu wa 2019/20 club ya Dar Salaam Young Africans leo ilikuwa Ndola Zambia kucheza mchezo wake wa marudiano dhidi ya Zesco.

Yanga wakiwa Zambia walikuwa wanaenda kwa lengo la kutafuta ushindi au sare ya kuanza magoli 2 na kuendelea ili waingie hatua ya makundi, hiyo inatokana na mchezo wao wa kwanza jijini Dar es Salaam.

Safari ya Yanga katika michuano hiyo imemalizika baada ya kufungwa 2-1 na kuondolewa kwa aggregate ya 3-2, magoli ya Zesco leo yamefungwa na Jesse Were dakika 24 na Makame wa Yanga aliyejifunga dakika ya 78 wakati goli pekee la Yanga lilifungwa dakika ya 30 ya mchezo na Sadney.

Yanga kutokana na kutolewa katika round hiyo sasa anadondokea michuano ya Kombe ka shirikisho Afrika huku aksubiri kumjua mpinzani wake katika hatua moja ya mtoano kabla ya kuingia Makundi.

Soma na hizi

Tupia Comments