Top Stories

Kondom zakutwa zimeanikwa juani

on

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile ameagiza Polisi wawakamate Watumishi wawili wa Hospitali ya Wilaya ya Rungwe kwa wizi wa dawa na utunzaji mbovu wa dawa pamoja na kondomu.

Naibu Waziri amechukizwa na kitendo cha Mfamasia wa Hospitali hiyo Eliah Kandonga kuanika kondomu juani akidai anataka kuzirejesha katika ubora wake baada ya kuona zinaharibika.

“Ni kosa kubwa hili, unawezaje kuhifadhi kondomu kwa kuzianika juani!, zinaharibika hata kuwa chanzo cha ongezeko la VVU, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Rungwe pia asimamishwe”– Ndugulile

MKANDARASI KAKIMBIA NA MILIONI 100 “APATIKANE MZIMA AMA AMEKUFA”

Soma na hizi

Tupia Comments