Shirika la Vijana la Young and Ilive initiative limewataka vijana kushiriki katika kongomano la ‘Young and Alive Summit 2024’ linalo lenga kuwaleta pamoja vijana, viongozi na wadau mbalimbali katika kujadili masuala muhimu ya vijana na mustakabali wao.
Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Young and Ilive Initiative, Sesilia Shirima katika uzinduzi wa kongamano la ‘Young and Ilive Summit’ linaloandaliwa na shirika la vijana la Young and Ilive na kutarajiwa kufanyika Tarehe 26 hadi 29 Novemba mwaka huu katika mkoa wa Arusha.
Aidha Sesilia amesema kuwa kongamano la mwaka huu lita lenga kuhimiza mashirikiano yaani (intergenerational Collaboration) kati ya vijana viongozi, wadau na Serikali ili kuleta matokeo chanya kwa ustawa wa vijana nchini.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji, Young & Alive Initiative , Bw. Otuck William amesema kongamano hilo lina tija kubwa kwani kupitia kongamano lililopita limeleta matunda kwa uwepo wa vijana waliofanikiwa kubadirika hivyo kwa kongomano la mwaka huu litakuwa ni fursa mno kwa vijana endapo wataudhulia mkoani Arusha.
Kwa Upande wake mnufaika kupitia kongamano lililopita Nasra Ramadhan amewataka vijana kutuma maombi ya kushiriki kongamano hilo na ili kuweza kujifunza mafunzo mbalimbali na kupata fursa zitazoweza kuwasaidia katika shughuli za kila siku.