Habari za Mastaa

Khadija Kopa ameeleza hapa kwanini imeshindikana kufanya wimbo wa pamoja na Mzee Yusuph

By

on

kopaLeo kupitia kipindi cha Leo Tena kutoka Super Brand Radio Clouds Fm Malkia wa mipasho Tanzania bi.Khadija Kopa ameelezea sababu zinazofanya kuchelewa kwa Collabo yake na Mzee Yusuph wa Jahazi Moderm Taarab.

yusAkijibu swali aliloulizwa kuhusu wasanii anaopenda kufanya nao kazi Bi.Khadija Kopa alitaja kuwa moja kati ya anaotegemea kufanya nao kazi ni pamoja na Mzee Yusuph ingawa alishawahi kumuomba wafanye hivyo mara mbili lakini amekua akijibiwa na mzee yusuph kuwa watafanya tu.

‘Sijui ni kitu gani lakini nilishawahi kumwambia mimi mwenyewe binafsi baadae marehemu mume wangu ambaye kipindi kile ndiyo alikua meneja wangu,akasema nitazungumza nae pengine labda wewe mke wangu hujazungumza nae vizuri’

‘Ikawa akipigiwa anasema sawa sawa,sasa ukiona mtu anadharau huwezi kumg’ang’aniza nahisi hapendi au muda hana,unajua mtu ukiona mtu kadharau huwezi kumg’ang’aniza mi nahisi hapendi ila hawezi kusema moja kwa moja’.

Tupia Comments