Korea Kaskazini imefyatua kombora la masafa ya kati kuelekea katika pwani ya mashariki na kaskazini wa Japan, jaribio ambalo limekosolewa vikali kimataifa.
Waziri anayehusika na kusimamia sera za baraza la mawaziri la Japan, Hirokazu Matsuno amesema kombora hilo limeangukia katika Bahari ya Pasifiki umbali wa kilomita 3,000 kutoka kwenye kisiwa cha Hokkaido na Mkoa wake wa kaskazini mashariki wa Aomori.
Matsuno amesema wamekusanya taarifa kuhusu ndege na meli zilizokuwa zinasafiri kwenye maeneo ya karibu kwa wakati huo lakini hakuna madhara yoyote yaliyotokea.
Amesema vitendo vinavyofanywa a Korea Kaskazini ikiwemo kurusha makombora mara kwa mara vinatishia amani na usalama wa chi vao na jumuia vote ya kimataifa na kwamba kufanya hivyo kunakiuka Azimio la Baraza la Usalama.