Wakala wa ujasusi wa jeshi la Korea Kusini umewaambia wabunge hivi leo kwamba Korea Kaskazini huenda imekamilisha maandalizi ya kufanya jaribio lake la saba la nyuklia na inaonekana inajiandaa kufanya jaribio la kombora la masafa marefu linaloweza kufika hadi Marekani.
Mmoja wa wabunge waliohudhuria kikao hicho, Lee Seong.kweun, amesema wakala wa ujasusi wa Korea Kaskazini unaamini umekamilisha maandalizi kufanya jaribio la nyuklia katika eneo la kufanyia majaribio hayo katika mji wa kaskazini mashariki wa Punggye-ri.
Korea Kaskazini yakosoa luteka za kijeshi za Korea Kusini, Japan na Marekani
Katika kikao cha ndani, wakala huo umesema vikosi maalumu vya Korea Kaskazini vilivyopelekwa nchini Urusi huenda wamefika katika maeneo ya vita huku vikosi hivyo vikijiandaa kwenda katika eneo la Kursk, ambako Urusi imekuwa ikipata shihda kudhibiti uvamizi wa Ukraine.