Top Stories

Kifo cha Waziri wa Ulinzi Korea Kaskazini kisa kasinzia mbele ya Rais.

on

koreSerikali ya Korea Kaskazini imeingia kwenye headlines baada ya waziri wake wa Ulinzi Hyon Yong-chol kuuawa wakati kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un alipokuwa akiwahutubia kwenye kambi ya kijeshi.

Taarifa iliyotolewa na Bunge la nchi hiyo inasema Waziri huyo alikumbwa na umauti baada ya kupigwa na kombora la kivita la kuangusha ndege mbele ya maafisa wakuu wa serikali wakati aliposinzia wakati mkutano huo ukiendelea.

woteHyon Yong-chol aliteuliwa kuwa mkuu wa jeshi la Korea Kaskazini  mwaka 2012 ambapo inasemekana alisinzia katika hafla iliyokuwa ikihutubiwa na Rais wa nchi hiyo na ni jambo ambalo lilimuudhi Rais.

Naona BBC wameripoti pia kwamba ukweli wa ripoti hiyo haujabainika kutokana na usiri wa serikali ya Korea Kaskazini ambapo idara ya ujasusi ilisema viongozi wakuu kwenye serikali wamekuwa wakiuawa kila mmoja kwa wiki.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye TwitterFacebook na Instagram kwa kubonyezahapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahaukusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video yaAyoTVikufikie

Tupia Comments