Nimekutana na stori kwenye mitandao, yenyewe inahusiana na ubunifu kwenye vitu vidogo tu mtu wangu. Kwa mfano ulishawahi kujiuliza ingekuaje kama kungekuwa na mwavuli unaokuruhusu kutuma na kupokea message wakati unatembea kwenye mvua!?
Yes mtu wangu ni kitu kidogo lakini kinawezekana! Wakorea wamekuja na ubunifu mpya wa miavuli wenyewe unaitwa Phone Umbrella maarufu kama ‘Phone-brella’ ambao unakuwezesha kwa urahisi kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja, kutuma message kwenye mvua na kujikinga na mvua ukiwa unatembea.
Phone-brella una kishikio kinacho valiwa mkononi kuupa mwavuli huo balance nzuri bila kuuchosha wala kuumiza mkono wako huku unatuma au kupokea message zako kwenye mvua bila kukupa shida yoyote ile yani.
Ubunifu huu umenifurahisha kwani ni kitu kidogo kilicho buniwa kwa akili ya utundu sana!, na hizi ni baadhi ya picha nilizoweza kuzinasa…
Hapa chini nimekusogezea video fupi inayo onyesha mwamvuli huo na jinsi unavyotumika karibu ujionee mtu wangu.
https://youtu.be/70pX5wia8ts
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos