Mix

Korea wamekuja na hii miavuli inayokuruhusu kutuma meseji kwenye mvua mtu wangu! + (Video).

on

umbr1

Nimekutana na stori kwenye mitandao, yenyewe inahusiana na ubunifu kwenye vitu vidogo tu mtu wangu. Kwa mfano ulishawahi kujiuliza ingekuaje kama kungekuwa na mwavuli unaokuruhusu kutuma na kupokea message wakati unatembea kwenye mvua!?

umbr2

Yes mtu wangu ni kitu kidogo lakini kinawezekana! Wakorea wamekuja na ubunifu mpya wa  miavuli wenyewe unaitwa Phone Umbrella maarufu kama ‘Phone-brella’ ambao unakuwezesha kwa urahisi kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja, kutuma message kwenye mvua na kujikinga na mvua ukiwa unatembea.

phone brella6

Hiki ndio kishikio cha mkono wa mwavuli huu wa Phone-brella.

Phone-brella una kishikio kinacho valiwa mkononi kuupa mwavuli huo balance nzuri bila kuuchosha wala kuumiza mkono wako huku unatuma au kupokea message zako kwenye mvua bila kukupa shida yoyote ile yani.

Ubunifu huu umenifurahisha kwani ni kitu kidogo kilicho buniwa kwa akili ya utundu sana!, na hizi ni baadhi ya picha nilizoweza kuzinasa…

phone brella3

Ukiutazama kwa haraka haraka unaweza kusema ni mwavuli tu wa kawaida.

phone brella4

Kishikio cha mwavuli kinaingia hapa kwenye mkono mtu wangu.

phone brella5

Ukishauvaa mwavuli wako mkononi , mwavuli utakaa hivi baada ya hapo ni wewe na message tu.

phone brella 8

Mwavuli huu unakuja kwenye rangi tofauti mtu wangu,yani hapo unachagua rangi uipendayo.

phone brella8

Mfuko wake pia uko tofauti na mifuko ya miavuli tuliyoizoea , plastic ya mfuko huu ni ngumu.

Hapa chini nimekusogezea video fupi inayo onyesha mwamvuli huo na jinsi unavyotumika karibu ujionee mtu wangu.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments