Japo headlines za siasa zilionekana kubeba uzito mkubwa miezi michache iliyopita, bado kuna mengine yaliendelea kwenye upande mwingine ikiwemo ishu ya ugonjwa wa kipindupindu ambao umeendelea kuripotiwa kwenye mikoa mbalimbali Tanzania.
Ripoti iliyonifikia leo inaonesha idadi ya wagonjwa waliougua kipindupindu mpaka sasa ni watu 10,412 huku ripoti ikionesha wengine 159 kuwa wamefariki baada ya kuugua… bado kipindupindu kipo, wagonjwa 97 bado wamelazwa katika maeneo mbalimbali.
Taarifa ya habari kituo cha ITV imesema maeneo yanayoongoza kuwa na wagonjwa wengi kwa sasa ni Kyela Mbeya ambako kuna wagonjwa 34, Arusha Mjini wagonjwa 11 na Ilemela Mwanza kuna wagonjwa 7.
Taarifa yote ya Habari ITV hii hapa ikiwa na ripoti yote.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.