Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo amesema kazi za kuwatumikia Wananchi hazihitaji ujuaji wala Mtu kujifanya mzoefu bali zinahitaji kusikiliza na kudumisha ushirikiano na kusema Mtu akijifanya Mzoefu huwa ndio mwanzo wa kuharibu kazi na Mtu akijifanya Mjuaji ndio mwanzo wa kufukuzwa.
Akiongea leo baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Basilla Mwanukuzi, Jokate ameahidi kuendeleza mazuri yaliyoanzishwa na DC Basilla huku akiwaomba Wananchi wampe ushirikiano.
“Dada yangu Basilla niseme Mimi nikuahidi, umenikabidhi hapo yale ambayo umeyafanya ukiwa Korogwe na wewe ulipokea kutoka kwa Dada yetu DC Kissa, yale yote ambayo yana manufaa kwa Wilaya yetu Mimi nitayaendeleza, kikubwa utaendelea kutushauri kama kuna ya msingi yenye manufaa, naamini DC au Kiongozi yoyote akianzisha jambo sio kwa ajili ya manufaa yake binafsi ni kwa manufaa ya Jamii anayoitumikia kwa wakati ule”