Habari za Mastaa

Kunani kati ya Karruache na mchezaji mpya wa Man United? Chris Brown katajwa pia! 

on

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Manchester United Memphis Depay, anaweza kujiingiza kwenye malumbano na muimbaji Chris Brown baada ya jana usiku kupost picha akiwa katika pozi tata na ex girlfriend wa muimbaji huyo, Karrueche Tran.

 Depay ambaye amesajiliwa na United mapema mwezi uliopita, kwa sasa yupo mapumzikoni nchini Marekani ambapo ndio amekutana na Karruache.

Ikumbukwe wiki kadhaa zilizopita mwanamitindo mkongwe Tyson Beckford aliingia kwenye malumbano na muimbaji Chris Brown baada ya mwanamitindo huyo kupost picha ya ‘selfie’ akiwa na mwanadada Karrueche Tran.

Chris Brown amekuwa na kasumba ya kugombana na kila mwanaume ambaye anakuwa na ukaribu na Karrueche, alianza na Drake na kisha Tyson Beckford.

Depay ambaye anatarajiwa kujiunga rasmi na timu yake mpya mapema mwezi ujao, alipost picha hiyo na Karruache na hakuandika caption yoyote huku akiwaacha mashabiki wake wakimsifia kwamba anapendezana na Msichana huyo huku wengine wakimuonya juu ya Chris Brown.

millardayo.com inaendelea kumtafuta Ben kwa ajili ya kujua taarifa zaidi kwenye ajali waliyoipata jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments