Michezo

KRC Genk baada ya kumfukuza Felice Mazzu, leo imetangaza kocha mpya

on

Uongozi wa club ya KRC Genk wiki iliyopita kuamua kumfuta kazi aliyekuwa kocha wao mkuu Felice Mazzu kwa kuwa na matokeo mabovu, leo club hiyo imemtangaza Mr Hannes Wolf kuwa ndio kocha mpya wa KRC Genk.

Felice Mazzu anaondoka Genk akiwa kadumu kwa miezi mitano tu huku akiiacha timu hiyo nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi ya Ubelgiji wakati ambao imepoteza matumaini ya kutetea Ubingwa wake wa Ligi Kuu ilioutwa msimu uliopita.

“KRC Genk inajivunia kutangaza kocha mpya Hannes Wolf leo atafundisha katika mazoezi yake ya kwanza” taarifa iliyotolewa na club hiyo.

Mr Hannes Wolf amewahi kufundisha vilabu mbalimbali ikiwemo Stuttgart aliyoipandisha daraja 2019, kabla ya kujiunga na Hamburg October 2018 lakini alifutwa kazi kwa kushindwa kufiia malengo ya kuipandisha Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga).

VIDEO: BONDIA ARNEL TINAMPAY NAMBA 2 KWA UBORA PHILIPINE BAADA YA MANNY PACQUIAO KATUA DSM

Soma na hizi

Tupia Comments