Ikulu ya Kremlin inasema kwamba ingawa inajua Papa Francis anafikiria kuhusu njia za kumaliza mzozo huo, haifahamu mipango yoyote ya kina ya amani kutoka Vatican.
Francis alisema Jumapili iliyopita kwamba Vatikani ilihusika katika misheni ya amani kujaribu kutatua mzozo huo lakini “haujaonekana hadharani”.
“Tunajua kwamba papa anafikiria mara kwa mara kuhusu amani, na tunajua kwamba papa anafikiria jinsi mzozo huu unaweza kukomeshwa,” msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema.
“Lakini hatufahamu mipango yoyote ya kina ambayo imependekezwa na Vatican katika muktadha huu,” alisema.
Papa Francis alisema Jumapili kwamba amefanya kazi katika mpango wa siri wa amani kati ya Ukraine na Urusi, zaidi ya miezi 14 baada ya uvamizi kamili wa Urusi tena.
Lakini wakati matarajio ya mapatano ya amani ya Papa yamezingatiwa katika siku za hivi karibuni, viongozi wa serikali ya Ukraine na Urusi na Kanisa wanasema hawajui kuhusu mpango wa Papa.
Papa Francis hakutoa maelezo yoyote lakini aliwaambia waandishi wa habari waliokuwa wakisafiri naye kwamba “anataweza kufanya chochote” ili kuleta suluhu iliyojadiliwa.