Kremlin imekanusha ripoti kwamba Vladimir Putin alipendekeza kusitishwa kwa mapigano nchini Ukraine kwa Marekani kupitia waamuzi.
Alipoulizwa ikiwa ripoti ya Reuters kwamba Urusi ilitoa mapendekezo ya amani ni kweli, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema: “Hapana. Si kweli.”
Ripoti ilisema nini?
Vyanzo vya habari vya Urusi vililiambia shirika la habari la Reuters kwamba Bw Putin alituma ishara mwaka jana kwa Washington hadharani na kwa faragha kupitia waamuzi, ikiwa ni pamoja na washirika wa Kiarabu wa Moscow katika Mashariki ya Kati, kwamba yuko tayari kufikiria kusitisha mapigano nchini Ukraine.
Waamuzi walikutana nchini Uturuki mwishoni mwa 2023, kulingana na vyanzo vitatu vya Urusi, na mshauri wa usalama wa kitaifa wa White House Jake Sullivan aliwasiliana na mshauri wa sera ya kigeni wa Bw Putin, Yuri Ushakov, mnamo Januari.
Ripoti hiyo ilisema Bw Putin alikuwa anapendekeza kusimamisha mzozo katika mstari wa sasa na hayuko tayari kuachia eneo lolote la Ukraine linalodhibitiwa na Urusi.