Stori Kubwa

Familia ya Bobby Brown yathibitisha kifo cha Bobbi Kristina… #RIP (Video)

on

bobi kristina

Imepita miezi sita toka Bobbi Kristina mtoto wa marehemu Whitney Houston akutwe amepoteza fahamu bafuni kwake, na toka kipindi hicho amekuwa kwenye coma kwa muda mrefu hospitalini kabla ya familia yake kumhamishia nyumbani baada ya kuona hakuna matumaini ya ziada.

Familia ya Bobbi Kristina imeweka wazi kuwa mtoto pekee wa marehemu Whitney Houston amefariki 27 July 2015 baada ya kipindi kirefu cha kuwekwa chini ya uangalizi wa madaktari.

Wanafamilia hao wana majonzi makubwa hasa wakiangalia kifo cha Bobbi ambavyo kimefanana kabisa na jinsi ambavyo mama yake mzazi, Whitney Houston alifariki.

Mipango ya mazishi yake inaendelea kufanywa, lakini kwa Nick Gordon huu ni wakati mgumu zaidi kwake kutokana na kushtakiwa kuwa mtu aliyehusika kutengeneza mazingira ya kifo cha Bobbi Kristina.

>>> “Sasa hivi tunataka kumzika binti yetu ili ampumzike kwa amani, lakini upelelezi mzito utaanza rasmi baada ya mazishi haya, yoyote yule aliyehusika kumsababishia mwanangu yote haya lazima mkono wa Sheria umpitie”. <<< Bobby Brown, baba wa Bobbi Kristina.

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments