Habari za Mastaa

Hii ni picha ya pili aliyoiweka Kelly Rowland inayomwonyesha mtoto wake

on

camera_hd_wallpaper_4 modifiedHivi unakumbuka vizuri picha ya kwanza ya staa mtoto Blue Ivy tumeiona muda gani baada ya mtoto huyo kuzaliwa? Imekuwa ni kawaida mastaa wengi kuwa na tabia ya kuficha sura za watoto wao kwa muda mrefu baada ya kuzaliwa watoto wao.

Ikiwa ni wiki tatu tangu ajifungue mtoto wa kiume, msanii Kelly Rowland ameweka kwa mara nyingine picha ya inayoonyesha miguu ya mtoto wake ambapo bado hakuna picha inayoonyesha sura yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram (@kellyrowland) ameweka picha ya miguu ya mtoto wake huyo pamoja na maneno haya; “…The most Happiest moment of my life — TJW! Share your Happiest moment now on Instagram using #ThisIsMyTime for a chance to win my new @twsteeltimepiece! –xo” @kellyrowland.

Hii itakuwa picha ya pili msanii huyo kushare kwenye mtandao wa Instagram.

Kelly Rowland ii Kelly Rowland

Hii ndiyo picha ya kwanza ambayo Kelly aliiweka ikimwonyesha mtoto wake.

Ni ahadi yangu kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments