Michezo

Hiki ndicho kiasi cha fedha atakacholipwa Toni Kroos ikiwa atajiunga na Man United

on

Arsenal-v-FC-Bayern-Muenchen-UEFA-Champions-League-Round-of-16-3163990Inaaminika kwamba Manchester United wapo tayari kumpa ofa ya mshahara wa £250,000 Toni Kroos ikiwa kiungo huyo wa kijerumani ataamua kuondoka Bayern Munich na kujiunga na kikosi cha David Moyes.

Mshahara wa £1million kwa mwezi ni mara tatu ya fedha anayolipwa Kroos hivi sasa na Bayern, ambaye inaaminika watahitaji kiasi cha £30m kama ada ya uhamisho kumruhusu mchezaji huyo kuondoka Allianz Arena baada ya kugoma kukidhi mahitaji mapya ya mshahara ya mchezaji huyo. 

Bayern kupitia kocha wao Pep Guardiola tayari alishasema kwamba wanataka kubaki na mchezaji huyo lakini akaongeza lolote linaweza kutokea – Bayern wana utajiri mkubwa wa viungo kwenye timu yao hivyo kumuuza Kroos kunaweza kusipunguze ubora wao.

Tupia Comments