Bomoabomoa iliyoanza mwishoni mwa mwaka 2015 kwenye baadhi ya maeneo jijini Dar es salaam hasa ya mabondeni ikiwemo maeneo yaliyo kando na mto msimbazi ambapo zoezi hilo lilisitishwa baada ya kesi inayopinga ubomoaji wa nyumba takribani 2619 za wakazi wa Tabata Segerea kufunguliwa.
April 22 2016 yametolewa maamuzi ya kesi hiyo ambapo Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi imesema kwamba kesi hiyo imekosa vigezo vya kisheria kutokana na kutokuwa na kibali cha wananchi wote kwa pamoja kinachoruhusu watu nane kufungua kesi badala ya wananchi wote.
Ayo TV imezungumza na Diwani kata ya Tabata, Patrick Assenga na wakili upande wa utetezi Abubakar Salim ambapo wamesema …..
>>>’kwahiyo tunaweza tukaenda tukaongeza hayo maneno wanayosema hayapo tukarudisha tena au tunaweza watu wote hawa 2619 wafungue kesi moja ambayo itakuwa ni ngumu, tutajipanga tujue nini tufanye kati ya hayo matatu’:-Abubakar Salim
>>>’sisi tunaenda kujipanga tutarudisha hii kesi kwa sababu nyumba 2619 ni watu wengi sana ambapo kuna takribani ya watu elfu arobaini na kitu hao watakosa makazi, Rais lazima aingilie kati ni suala kubwa na limebeba maslahi ya watu wengi’:-Patrick Assenga
ULIIKOSA VIDEO YA BOMOABOMOA YA NYUMBA KINONDONI DEC 17 2015? ANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE