Habari za Mastaa

Maneno ya Madee, Dogo Janja baada ya BASATA kusema hakuna tuzo za KTMA

By

on

Baada ya Baraza la Sanaa Tanzania ‘BASATA’ kusema mwaka huu pia hakutokuwa na tuzo za Music Tanzania maarufu kama Kilimanjaro Music Award (KTMA) staa wa muziki Madee amekosoa hatua hiyo.

Madee aliandika kwenye account yake ya Twitter akisema: >>>“Muziki wetu umepata kilema, hauna tuzo hauna album halafu kuna watu wanasema wanataka kuufikisha mbele, hahaha kwa njia gani labda” – Madee.

Baada ya tweet ya Madee naye Dogo Janja aliandika kwenye Instagram >>>”Tunataka mashindano yakimataifa bila kua na shindano la kitaifa hahaha tutapigwa nyingi daily” – Dogo Janja.

VIDEO: BASATA kuhusu Tuzo za muziki Tanzania ‘KTMA’ 

VIDEO: Roma Mkatoliki ameongea kuhusu kuonekana akifundisha shule ya msingi. Bonyeza play kutazama!!!

Soma na hizi

Tupia Comments