Takwimu zilizotolewa na idara ya Marekani ya Kilimo (USDA) zimeonyesha kwamba nchi zilizoendelea zina asilimia ndogo ya matumizi ambayo hutumika kwa ajili ya chakula kwenye familia ukilinganisha na nchi ambazo zinazoendelea.
Takwimu hizo zimeeleza kuwa katika nchi ambazo zinatumia zaidi kipato cha familia kwa ajili ya chakula ni pamoja na Nigeria ambayo imetajwa kutumia zaidi ya nusu ya kipato cha familia kwa ajili ya chakula ambapo pia kuna nchi zaidi ya tisa ambazo zimetajwa kutumia zaidi ya 40% ya kipato cha familia kwa ajili ya chakula.
Kwa Afrika zipo nchi nne kwenye hiyo list ambapo ni Nigeria 56.4%, Kenya 46.7%, Cameroon 45.6%, na Algeria 42.5% lakini nje ya Afrika ni Kazakhstan 43.0%, Philippines 41.9%, Pakistan 40.9%, Azerbaijan 40.1%. Guatemala 40.6%.
Takwimu hizo zimeeleza kuwa kuna nchi nane ambazo hutumia chini ya 10% pato la familia kwa ajili ya chakula, nne zipo Ulaya ambazo n i pamoja na Uingereza ambayo ni ya tatu ikiwa na 8.2% ikifuatiwa na Uswisi kwa 8.7%, Ireland 9.6% na Austria 9.9%.
Mataifa mengine ni Marekani ambayo inatumia 6.45%, Singapore ni ya pili ikiwa na 6.7%, Canada ni 9.1 wakati Austria 9.8%.
ULIPITWA? Mfungwa Mtanzania aibia simu Gerezani China na kumpigia Millard Ayo, bonyeza play kwenye hii video hapa chini