Duniani

Rekodi nyingine ambayo Donald Trump anaiweka Marekani

on

Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump anatarajiwa kuapishwa January 20 2017, ushindi wa Donald Trump umetajwa kuwa wa kihistoria katika siasa za Marekani.

Wakati zikiwa zimebaki siku 10 Trump kuapishwa kitu cha kufahamu ni kwamba Trump anaiweka rekodi ya kuingia White House akiwa na umri mkubwa zaidi.

Trump ataapishwa kuwa Rais wa 45 wa Marekani akiwa na umri wa miaka 70, rekodi hiyo ilishikiliwa na Ronald Reagan ambaye aliingia White House akiwa na miaka 69 mwaka 1981.

Rais wa zamani wa Marekani, Theodore Roosevelt ndiye Rais aliyeingia madarakani akiwa na umri mdogo zaidi, Roosevelt alikuwa na miaka 42,  John F. Kennedy alikuwa mkubwa kidogo alipochukua madaraka miaka 60 baadaye akiwa na umri wa miaka 43.

trump

AyoMAGAZETI: DCI afunguka kutoweka kwa msaidizi wa Mbowe, Mabadiliko yaja Elimu ya msingi, Bonyeza play hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments