Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: BREAKING: Rais Magufuli afuta agizo la cheti cha kuzaliwa kwa watakaofunga ndoa
Share
Notification Show More
Latest News
Picha:Kutoka kwenye shangwe za Simba DAY uwanja wa Mkapa Dar es Slaam
August 8, 2022
Kizz Daniel kutotokea kwenye show, Str8upvibes watoa tamko
August 8, 2022
Watalii zaidi ya 30 watembelea maporomoko ya Maji Hululu
August 8, 2022
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 8, 2022
August 8, 2022
International Marathon yaacha historia Zanzibar
August 7, 2022
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > BreakingNews > BREAKING: Rais Magufuli afuta agizo la cheti cha kuzaliwa kwa watakaofunga ndoa
BreakingNews

BREAKING: Rais Magufuli afuta agizo la cheti cha kuzaliwa kwa watakaofunga ndoa

March 17, 2017
Share
2 Min Read
SHARE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelifuta agizo lililotolewa jana tarehe 16 Machi, 2017 na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe linalotoa sharti la kuwa na cheti cha kuzaliwa kwa watu wote watakaofunga ndoa kuanzia tarehe 01 Mei, 2017.

Rais Magufuli amefuta agizo hilo leo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi kabla ya kuondoka katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma na kurejea Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Magufuli amesema Serikali haiwezi kuruhusu sharti hilo kutumika kwa kuwa litawanyima haki ya kuoa na kuolewa Watanzania wengi ambao hawana vyeti vya kuzaliwa, huku utaratibu wa kupata vyeti hivyo ukiwa bado unakabiliwa na changamoto nyingi kwa wanaohitaji.

Amesema mpaka sasa idadi ya Watanzania walio na vyeti vya kuzaliwa ni chini ya asilimia 20 huku wengi wao wakiwa ni wananchi waishio vijijini ambako ni vigumu kupata vyeti hivyo, na wengine wakiwa ni waliozaliwa kabla ya kuanza kutolewa kwa vyeti vya kuzaliwa nchini mwaka 1961.

“Kwa hiyo ndugu zangu Watanzania msiwe na wasiwasi wowote, endeleeni na utaratibu wenu wa kuoa na kuolewa kama kawaida na kama kuna kifungu chochote cha sheria kinachomlazimisha mtu awe na cheti cha kuzaliwa ndipo aoe ama aolewe nitamuelekeza Waziri wa Katiba na Sheria Harrison Mwakyembe apeleke Bungeni kikarekebishwe”-Rais Magufuli.

Rais Magufuli ametoa wito kwa wanasheria kuziangalia vizuri sheria zinazohusiana na kuzaliwa na kifo na kuoa na kuolewa ili zisilete mkanganyiko kwa wananchi. Hata hivyo Mhe. Rais Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kupata vyeti vyao vya kuzaliwa kama kawaida na amewataka viongozi wote kuwahamasisha wananchi kuwa na vyeti hivyo.

VIDEO: Rais Magufuli alivyotembelea eneo la ujenzi wa Ikulu Chamwino Dodoma, Bonyeza play hapa chini 

Unazitaka Breaking NEWS na Stori zote? ungana na Millard Ayo kwenye Facebook Twitter Instagram na Youtube na atakuletea matukio yote ya picha, video na habari iwe usiku au mchana…. bonyeza hapa >>> FB Twitter Instagram YouTUBE.

You Might Also Like

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo September 29, 2021

Aliyezaa na Harmonize kafunguka kwa mara ya kwanza, adai Harmonize anamtumia mwanae

Polepole atangaza CCM kusimamia matibabu ya Wasanii waliopata ajali

BREAKING: Ruge Mutahaba afariki dunia

BREAKING: Watu 7 wafariki gari la CAG na la PSSSF yakigongana uso kwa uso

TAGGED: Breaking news
Edwin Kamugisha TZA March 17, 2017
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article AyoTV MAGAZETI: Bulembo afichua mil 40 alizopewa na Lowassa, Meya kumshtaki Makonda
Next Article VIDEO: MC Pilipili asimulia alivyochekesha, watu hawakucheka Kahama ikabidi aondoke
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Picha:Kutoka kwenye shangwe za Simba DAY uwanja wa Mkapa Dar es Slaam
Mix August 8, 2022
Kizz Daniel kutotokea kwenye show, Str8upvibes watoa tamko
Top Stories August 8, 2022
Watalii zaidi ya 30 watembelea maporomoko ya Maji Hululu
Mix August 8, 2022
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 8, 2022
Magazeti August 8, 2022

You Might also Like

Magazeti

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 7, 2022

August 7, 2022
Magazeti

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 6, 2022

August 6, 2022
Magazeti

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 5, 2022

August 5, 2022
Magazeti

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 4, 2022

August 4, 2022
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?