Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro leo July 5, 2017 amepokea msaada wa magari manne kutoka Kampuni ya Great Wall Motor ya China ambapo wakati anapokea magari hayo amesema magari hayo yatasaidia kupunguza changamoto za Polisi.
Aidha, IGP sirro aligusia kuhusu issue ya matukio ya mauaji yanayoendelea maeneo ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji katika Mkoa wa Pwani ambapo amewataka wananchi wa maeneo hayo ambayo pikipiki ya Polisi haiwezi kupita wajilinde kwa kuimarisha ulinzi shirikishi.
ULIKOSA? Wizara Mambo ya Ndani, IGP Sirro wazungumza kuhusu mauaji Kibiti, Bonyeza play hapa chini kutazama