Burudani

VIDEO: Sababu za Wolper kukatwa kuwa Jaji Miss Lake Zone

on

Leo August 27 2018 kamati ya maandalizi ya Miss Tanzania 2018 wamekutana na waandishi wa habari kuzungumzia mwendelezo wa mashindano hayo ambapo moja ya swali lililoibuliwa na waandishi wa habari ni kuhusu mwigizaji Jackline Wolper kuondolewa kwenye list ya watu ambao walitakiwa kuwa majaji wa Miss Lake Zone.

Akijibu Swali hilo Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look  ambao ni Waandaaji wapya wa Shindano la Miss Tanzania 2018, Basila Mwanukizi ametaja sababu za Mwigizaji Jackline Wolper kutokidhi vigezo kuwa miongoni Majaji wa shindano la Miss Lake Zone ……….

‘Ni utovu wa nidhamu wa waandaaji wa miss lake zone, kuna taratibu waandaji wanapewa, majaji wanapewa semina, Wolper alichelewa kufika kwenye semina ataingiaje kujaji hajaongozwa hajui anajaji nini? sio tu uwe superstar uje kujaji, kuna miongozo maalumu’

LIVE: Waandaji wa Miss Tanzania 2018/ Rushwa za Ngono/ Kila Mtu anamshindi wake, Bonyeza play hapa chini kutazama

Tupia Comments