Michezo

Baada ya kutolewa Champions League, Real Madrid wamepata pigo jingine

on

Wakatia club ya Real Madrid pamoja na mashabiki wao wakiwa katika majonzi mazito kutokana na timu yao kuondolewa mapema katika michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2018/2019 tofauti na ilivyozoeleka, kuna habari mbaya pia imeripotiwa leo kuhusiana na moja kati ya wachezaji wao ambaye wanamtegemea pia.

Club ya Real Madrid leo imepokea taarifa za kuthibitika kuwa itamkosa kwa miezi miwili Vinicius Jr, hiyo inatokana na staa huyo kupata majeraha wakati wa mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League dhidi ya Ajax mchezo ambao umemalizika kwa Real Madrid kuvuliwa Ubingwa na kuaga rasmi michuano hiyo 4-1 (agg 5-3).

Jeraha alilolipata Vinicius Jr mwenye umri wa miaka 18 kitaalam linajulikana kwa jina la torn ligaments, kama utakuwa unakumbuka vizuri Vinicius Jr alijiunga na Real Madrid 2018 akitokea Flamengo lakini amepata jeraha kubwa litakalomuweka nje kwa kipindi cha miezi miwili

Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake

Soma na hizi

Tupia Comments