September 4 2017 mamlaka ya hali ya hewa kupitia kwa mkurugenzi Mkuu wake, Dk. Agnes Kijazi amekutana na wanahabari kutoa taarifa kuhusu mweleko wa mvua za vuli.
Dk. kijazi amesema mvua za vuli 2017 zinatarajiwa kuanza mwezi September katika maeneo mengi ya ziwa viktoria na mwezi october 2017 katika ukanda wa Pwani na baadaye mwezi November katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki.
Aidha Dk. Kijazi amesema ongezeko la mvua linatarajiwa katika miezi ya November na December 2017 pia vipindi virefu vya ukavu vinatarajiwa kujitokeza zaidi katika mwezi october 2017. Unaweza kubonyeza play hapa chini kuitazam hii video hapa chini
Ulikosa? AyoTVMAGAZETI: Matukio 7 yaliyozua mjadala, Asimulia jinsi alivyowateka watoto 4 Arusha, Bonyeza play hapa chini kuitazama hii video