Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Chris Brown apinga shtaka alilofunguliwa, aapa kutoa ushahidi

on

Mtandao wa ‘The Blast’ umeripoti kuwa mwimbaji wa miondoko ya RnB Chris Brown ameapa kuonyesha ushahidi wa mwanaume ambaye alimfungulia mashtaka na kusema kuwa alimpiga ngumi. CB alikanusha shtaka hilo na kudai kuwa hakufanya kitendo hicho.

Kwa mujibu wa makala kutokea Mahakamani umedai kuwa Chris Brown ataonyesha ushahidi wa Bennie Vines siku ya May 31,2019 kuwa hakufanya kitendo hiko na imeelezwa kuwa wakati wa ushahidi CB ataruhusiwa kujitetea kuhusu kosa aliloshtakiwa la kumpiga ngumi katika kumbi ya starehe ya Tampa nightclub Marekani mwaka 2017.

Inaripotiwa kuwa Bennie Vines aliajiriwa kupiga picha matukio mbalimbali katika club hiyo lakini Chris Brown alionekana kupinga kile alichokuwa akifanya Vines na hivyo kuamua kumvamia na kumpiga ngumi ya mdomo lakini baadae CB alifunguliwa shtaka kwa kufanya hivyo.

VIDEO: MOSE IYOBO HAJATOKEA KWENYE BIRTHDAY YA MWANAE, AUNT EZEKIEL KAZUNGUMZA

Soma na hizi

Tupia Comments