AyoTV

VIDEO: Mbunge wa Ubungo akisimulia alivyokamatwa na Polisi kisa zile vurugu za uchaguzi wa Meya

on

Leo March 10 2016 Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), Saed Kubenea amehitajika polisi kwa tuhuma za kuhusika na vurugu  wakati uchaguzi huo ulipoahirishwa February 27 2016. Saed Kubenea ameelezea kuhusiana na wito huo wa polisi kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo na amesimulia ilivyokuwa…

Nimefuatwa na askari kama sita wakiniambia kwamba niko chini ya ulinzi ninahitajika makao makuu ya polisi Dar es salam nikahoji kosa langu ni nini? wakasema nikajibu tuhuma juu ya vurugu zilizotokea katika uchaguzi wa Meya wa Dar es salaam‘:-Saed Kubenea

’Mimi nilifika makao makuu polisi kuwasilisha malalamiko juu ya amri iliyotolewa kwamba uchaguzi ule uzuiliwe, niliwathibitishia Polisi kwamba amri ile ilikuwa haramu na ilikuwa imeexipire kwa hiyo ni lazima wachukue hatua za kisheria dhidi ya wahusika‘:-Saed Kubenea

Hii ndio video yake….

Kama uliimiss hii video ya Dakika 11 za vurugu zilivyotokea katika uchaguzi wa Meya Dar …

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTERFBYOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments