Mix

Hili ndilo basi lililochomwa moto na Wananchi Singida likiwa safarini.

on

Screen Shot 2014-01-09 at 9.07.49 PMHii ni ajali ambayo imetokea njia Panda ya kwenda Arusha kama unatokea Singida, wakazi wa eneo hilo wamechoma moto basi la Mtei ambapo millardayo.com imeongea na miongoni mwa mashuhuda na abiria wa ajali hiyo na wametoa haya maelezo hapa chini.

mamteiAbiria mmoja ana sema ‘tumepandia pale stand ya Mwenge tulikua tunaenda Arusha na tulipofika hapa kuna abiria akasema kuna watu wamegongwa ndo tukashuka tukakuta kweli wamegongwa watu wanne hii pikipiki ilikua mbele alikua kapakia abiria watatu na yeye mwenyewe alikua wanne tulikua tunaongozana nae akataka kumpita akaona basi mbele linakuja akarudi akataka kumuova teki huyu dereva bodaboda’

‘Wanakijiji ndio wakapigiana simu wakaja hapa ndio wakasema tulichome moto hili  basi leo’

mteiKamanda wa Polisi Singida anasema ‘abiria wawili wa pikipiki walipoteza uhai papohapo na abiria wawili waliumia na kukimbizwa hospitalini mpaka sasa taarifa tulizonazo ni kwamba  abiria mmoja ambaye alikua amejeruhiwa na kukimbizwa hospitalini amefariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu hivyo jumla ya waliofariki ni watatu’

‘basi hilo limeteketea sehemu ya juu yote ya kukaa abiria na sehemu ya chini imeharibika kutokana na joto ambalo lilikuwa linatokea juu, tukio limetokea leo saa moja asubuhi katika kitongoji cha Ijanuka kijiji cha Kisasida’

Basi hili mali ya kampuni ya Mtei lenye namba za usajili T.742 ACU aina ya Scania lilikua likiendeshwa na Dismas Ludovick na lilikuwa linatoka Singida mjini kwenda Arusha mjini.

Kamanda Kamwela amesema lilipofika kitongoji cha Ijanuka ilitokea  pikipiki aina ya sky go yenye namba za usajili T368 BXZ iliyokuwa inaendeshwa na Shaban Bunku huku akiwa amepakia watoto wake wa kiume watatu ambapo ilikatisha ghafla kitendo kilichosababisha kugongwa na kuburutwa zaidi ya hatua 20.
‘Baada ya kutokea kwa ajali hiyo Dereva wa basi hilo alilazimika kusimamisha basi hilo kutokana na kuburuza pikipiki hiyo na baada ya kusimamisha basi wananchi wa eneo hilo walipigiana simu na ghafla walijaa na kuanza kuvunja vunja vioo na kisha kulichoma moto’- Kamanda  Kamwela.
Tayari polisi wameanzisha msako mkali wa kusaka wananchi waliojichukulia sheria mkononi ili kuwakamata waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

‘Tabia hii ya kujichukulia sheria mkononi haikubaliki, tutahakikisha tumewakamata wote waliohusika na uharibifu huu na
Sheria ipo wazi kwamba hata kama mtu kafanya kosa, wananchi hawaruhusiwi kabisa kujichukulia sheria mkononi’-Kamanda Kamwela.

Tupia Comments