Michezo

Kuelekea game ya Leicester vs Aston Villa, Mambo 5 kuhusu Samatta

on

leo usiku watanzania watapata nafasi tena ya kumtazama nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta akiicheze Aston Villa dhidi ya Leicester City saa tano usiku katika game ya EPL.

Hadi sasa toka Samatta awasili Aston Vila wamecheza game 5 na kushinda game mmoja na kati ya hizo Samatta kafunga magoli mawili leo usiku kuna jipya atafanya?

Hizi ndio rekodi nne za Samatta toka awasili Aston Villa January akitokea KRC Genk ya Ubelgiji kwa kiasi kinachokadiriwa kufikia au zaidi ya pound milioni 8.

1- Samatta hadi sasa ana rekodi ya kuwa ndio mchezaji wa kwanza wa Aston Villa kufunga goli la kichwa msimu wa 2019/20.

2- Samatta ndio mchezaji wa kwanza kuifunga timu inayofundishwa na Pep Guardiola katika mchezo wa fainali baada ya Rooney kufanya hivyo 2011 katika mchezo wa fainali ya UEFA.

3- Ni mtanzania wa kwanza kucheza EPL na kufunga goli katika game za EPL

4- Baada ya Samatta kufunga goli katika mchezo wa fainali ya Kombe la Ligi (Carabao Cup) vs Man City licha ya Aston Villa kupoteza 2-1, Samatta anakuwa muafrika watano kuwahi kufunga goli katika mchezo wa Ligi fainali ya Kombe la Ligi England baada ya Didier Drogba, Yaya Toure, Desire Job na Obafen Martins.

Soma na hizi

Tupia Comments