Jumamosi Julai 30, Taasisi ya Kizalendo ya Tanzania Patriotic Organization (TPO), imefanya Bonanza Kubwa la kuhamasisha Sensa ya watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23, Mwaka huu.
Mwenyekiti wa Taifa wa TPO, Hamad S Juliu ameongoza Bonanza hilo lililofanyika katika viwanja vya Stakishari Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali wa Taasisi hiyo.
Mwenyekiti Hamad S. Juliu amewasisitiza wananchi kujitokeza kuhesabiwa ifikapo Agosti 23 Mwaka huu, kwa kuwa Takwimu hizo sensa ndizo zinazo saidia serikali kupanga maendeleo ya nchi.
Pia Mwenyekiti Hamad S Juliu amesema Taasisi hiyo ya Kizalendo, itaendelea kumuunga Mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika jitihada mbalimbali za kukuza uchumi wa nchi, hivyo ndio maana wameamua kumuunga mkono Rais kwa kufanya bonanza hilo.
Aidha mbali na utolewaji wa elimu ya hamasa ya sensa, bonanza hilo lilihusisha michezo mbalimbali ikiwe Mpira wa Miguu, kukimbiza kuku, kubeba mayai kwa kijiko kutumia meno na burudani ya Muziki.
Bonanza hilo lilijumuisha wananchi mbalimbali wa kila rika zaidi ya 300 wakiwemo viongozi wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi(CCM).