Habari za Mastaa

Kufuatia tukio la Will Smith kumchapa kibao Chris Rock, Jada Smith kayaandika haya

on

Jada Pinkett Smith amevunja ukimya baada ya Mume wake Will Smith kukosolewa kwa kumpiga kibao Mchekeshaji Chris Rock kwa kufanya mzaha juu yake.

Jada ameandika kupitia akaunti zake mitandaoni “”msimu wa uponyaji” katika kile kinachoonekana anamaanisha tukio la Oscars.

Mume wake, Will Smith, ameomba msamaha siku ya Jumatatu, akitaja tukio hilo kuwa vurugu, sumu na uharibifu.

“Vurugu njia zote ni sumu na uharibifu, mwenendo wangu wa jana usiku katika Tuzo haukubailiki na hauna udhuru, utani ni sehemu ya kazi lakini mzaha kuhusu hali ya kiafya ya Jada ulikuwa mzito sana kwangu kuvumilia kihisia.”- Aliandika Will Smith
Tukio hilo la Jumapili usiku lilitokea kabla tu ya Smith kushinda tuzo ya Oscar ya Muigizaji Bora, wakati mchekeshaji Rock alipokuwa jukwaani kutoa tuzo ya Makala Bora kisha akamdhihaki Jada kwa kunyoa nywele, Jada ana ugonjwa unaosababisha nywele zake kukatikakatika.
MAPYA YAIBUKA BRIANA AWEKA WAZI KUHUSU HARMONIZE “NI KWELI TUMEACHANA, NITARUDI KUWATEMBELEA”

 

Tupia Comments