Top Stories

Kufumania ni mpaka uwe na cheti cha ndoa

on

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata watuhumiwa wanaoonekana kwenye video clip mitandaoni wakiwashambulia wapenzi wakiwa kwenye faragha kwa madai ya kwamba wamewafumania.

Simbachawene ametoa agizo hilo leo Agosti 6, 2021 Jijini Dar es Salaama mara baada ya kuiona video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikionesha kundi la watu wakiwavamia wapenzi hao na kuwadhalilisha kwa kuwapiga na kuwarushia maneno.

“Hivi karibuni kumejitokeza tabia ya baadhi ya watu ambao wanawavamia na kuingia katika maeneo ambayo watu wenye mahusiano ya kimapenzi wanakwenda kufanya faragha zao tabia hii ambayo imeshamiri sasa kama ambavyo clip nyingi zimekuwa zikirushwa rushwa nadhani leo nichukue nafasi kutoa msimamo wa kisheria na kukemea tabia hii ambayo imeanza kuota mizizi,” Waziri Simbachawene.

Soma na hizi

Tupia Comments